Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi Kinyasini mkoa wa Kaskazin Unguja kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya na bangi zenye viwango tofauti.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja Haji Abdallah Haji amesema operesheni wanazofanya katika maeneo tofauti ya mkoa huo ni kuweza kuwatia nguvuni wale wote watakaohusika na uhalifu wa kuingiza madawa ya kulevya.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Mtumwa Khamis mwenye umri wa miaka 25 ambae amekamatwa na kete 32 za unga aina ya Heroine zenye uzito 0.70 grams.

Mwengine Hamad Faki Makame mwenye umri wa miaka 28 ambae amekamatwa akiwa na misokoto ya majani makavu 30 yenye uzito wa 0.6 grams.

Sambamba na hayo Kamand Haji amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa  uchunguzi.

Young Africans yawaalika mabingwa wa Burundi
Kanda athibitisha kuondoka Simba SC