Mwalimu wa shule ya msingi, Ilembo B iliyopo manispaa ya Mpanda, George Masinge (47) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumfunga mnyororo shingoni na kumfungia ndani mkewake, Sababile Seif (75).

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limebainika Aprili 22, mwaka huu na jeshi la polisi linamshikilia pia mke wa mtuhumiwa huyo kwa mahojiano.

Amesema kuwa mama huyo alikutwa na askari polisi akiwa amefungiwa ndani nyumbani kwa mtuhumiwa huku akiwa amefungwa mnyororo shingoni ambao ulikuwa umefungwa kwenye nondo ya dirisha.

” Hata hivyo bado haijafahamika alikuwa amefungwa mnyororro shingoni kwa kipindi gani, japo mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alidai alimfunga hivyo mama mkwe wake kwakuwa alikuwa kichaa” Ameeleza kamanda Kuzaga.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya msamaria mwema kulitaarifu jeshi hilo huku akieleza kuwa mama huyo amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa katavi kwaajili ya matibabu.

Aidha amebainisha kuwa baada ya upelelezi kukamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Wanafunzi 2 familia moja, mwalimu wafa maji
Kim Jong-un aonekana hadharani, afanya hili kukiwa na tetesi kuwa amefariki