Mtu mmoja Janeth Dominick (26) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za shambulio la kudhuru mwili kwa kumwagia chai ya moto Dada wa kazi, Filomena Erick (17), akimtuhumu kuiba Simu, Sukari na Unga katika chumba cha jirani katika Nyumba waliyopanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Kamanda wa Polisi Mkoani Kibaha, ACP Pius Lutumo imesema tukio hilo limetokea Septemba 14, 2023 majira ya saa 2:00 asubuhi ambapo siku ya tukio mtuhumiwa alimuunguza mlalamikaji sehemu mbalimbali za mwili.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kibaha, ACP Pius Lutumo.

Tukio hilo lilitokea eneo la Kibaha kwa Mathias lililopo Mkoani Pwani, ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa mtuhumiwa ambaye ni mwajiri wa dada huyo wa kazi, alimuunguza maeneo ya Shingoni, Mkononi, Kifuani na Tumboni na kwamba vitu hivyo vinadaiwa kuibwa kwa chumba cha mpangaji mwenzao.

Aidha, taarifa ya Kamanda Lutumo imeendelea kufafanua kuwa, Mtuhumiwa huyo Janeth Dominick anatarajia kufikishwa kwenye mifumo ya kisheria mara baada ya upelelezi juu ya tukio hilo utakapokamilika, huku jamii ikikemea matukio kama hayo kwani havina utu na vina madhara na vinaleta chuki.

Harry Kane aipandisha Presha Man Utd
Cedrick Kaze kumfunga paka kengele?