Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Emuguru wilayani Same kwa tuhuma za kumuozesha binti yake mwenye umri wa miaka 11.
Akizungumzia na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa kilimanjaro Simon Maigwa, amesema kuwa tayari baba huyo alishapokea mahari ya ng’ombe watatu kutoka kwa muoaji.
Kamanda Maigwa amesema kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa alishafanya sherehe ya kimila Agosti 7, 2021 nyumbani kwake kumuaga binti huyo kwenda kwa mume wake.
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limetoa onyo kali kwa watu wenye tabia za kuozesha watoto wadogo chini ya umri wa miaka 18 kwani ni kinyume cha sheria.