Mwenyekiti wa Chama C cha NCCR Mageuzi James Mbatia ameipongeza Serikali kwa kulitambua janga la corona na kuchukua hatua za kuhamasisha na kuelimisha wananchi kujinga na janga hilo.
Amesema hayo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam.
Ambapo ameshauri kufanyika kwa tathmini ya corona nchini, itakayosaidia kuwekwa vipaumbele na usimamizi utakaosaidia kukabiliana na maambukizi zaidi.
Aidha, Mbatia amesema kuwa takwimu za ugonjwa wa corona Barani Afrika zinaonesha katika wimbi la tatu la ugonjwa huo kuna ongezeko la asilimia 43 ya maambukizi ikilinganishwa na wimbi la kwanza na la pili, hivyo tahadhari zaidi inahitajika.