Mkutano wa Wadau wa sekta ya Kilimo, umefanyika hii leo Desemba 5, 2023 Mjini Babati Mkoani Manyara, ukiwa na lengo la kutoa Elimu juu ya utambuzi na matumizi sahihi na mbegu Bora ya zao la Maharage.
Akifungua mkutano huo, Mgeni rasmi Afisa Kilimo Wizara ya Kilimo, Idara ya Maendeleo ya Mazao, Hamza Mohamed Nangameta amesema amepongeza ushirikiano katika mazao ya jamii ya mikunde kama vile Maharage na kusema watakahakikisha wanaweka mikakati katika utatuzi wa migogoro na changamoto mbalimbali katika sekta ya Maharage.
Akitoa neno la shukrani Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Twange ameiomba Wizara kuiweka Manyara katika swala la Kilimo kwa kuwa Wananchi wa Mkoa huo asilimia kubwa ni wakulima na Kilimo ni Biashara na Kilimo ni Sayansi.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural market Development (ADMT), Vicky Msamba amesema Taasisi hiyo imeanzishwa mwaka 2014 kwa ushirikiano bwa nchi tano ikiwemo Tanzania, ikiwa na lengo la kuratibu mambo mbalimbli ya kuendeleza na kuweka mifumo ya Kilimo sawa.
Amesema mpaka sasa wamefanya kazi Katika mazao makuu matatu, ambayo ni Mahindi, Maharage na Alizeti ikiwa wao kazi Yao kubwa kuangalia changamoto zilizopo kwenye mazao hayo pamoja na masoko Ili zao hilo liweze kukuwa vizuri na liweze kujitengemea na kumpa faida Mkulima.
Nao baadhi Wakulima walio hudhulia katika mkutano huo wamezungumzia juu ya uhaba wa upatikanaji wa mbegu umekuwa imekuwa tatizo kubwa hivyo ameiomba AMDT Kuweza kuwafikishia mbegu hizo hasa Kwa wakati pamoja na upatikanaji wa pembejeo Kwa ujumla.