Kikosi cha Mbeya City FC, kimesema kuwa ushindi katika mechi yao dhidi ya Yanga inayotarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi ni muhimu ili waweze kujiweka katika mazingira mazuri hasa kipindi hiki ligi ikielekea ukingoni.
 
Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten mara baada ya kuanza safari kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukabiliana na Yanga,
 
Amesema kuwa jumla ya wachezaji 18 na viongozi 10 watakuwa kwenye msafara huo kwa ajili ya kuhakikisha City inafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu.
 
“Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu na matarajio yatu ni kushinda na kupata matokeo muhimu kwenye mchezo wa jumamosi, kwani tunafahamu Yanga ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo halitupi hofu kwa sababu tunakikosi kikosi kizuri,”amesema Ten
 
Aidha, Ten amesema katika mzunguko wa kwanza waliweza kupata matokeo mazuri na sasa wanakwenda Jijini Dar kuhitimisha dhamira yao ya kupata pointi sita msimu huu kutoka kwao
 
Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo, Kinnah Phiri amesema hana wasiwasi na mchezo huo wa jumamosi kwa sababu anaifahamu vyema Yanga hasa baada ya kuifuatilia kwenye michezo kadhaa na tayari ameandaa mbinu za kuhakikisha vijana wake wanapata ushindi

Gereza la Wanawake Mpwapwa lafunguliwa, nyumba 9500 za Askari Magereza kujengwa
Kikosi Cha Serengeti Boys Chapitishwa CAF