BAADA ya mapumziko ya siku ya jana  yaliyotolwa na kocha Kinnah Phiri kufuatia  safari ndefu ya saa nyingi kutoka  kanda ya ziwa, kikosi cha Mbeya City fc  leo kimeanza mazoezi rasmi kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc  uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa  siku ya jumamosi.

Akizungumza na mbeyacityfc.com  mapema leo afisa  habari wa City, Dismas Ten  amesema kuwa  nyota wote 30 ikiwa ni pamoja na 25 waliokuwa nje ya jiji la Mbeya kwa takribani wiki tatu kwa ajili ya michezo ya mwanzo wa msimu wamejumuika kwenye mazoezi ya leo kwenye uwanja wa Sokoine kwa ajili ya matayarisho ya mchezo huo wa mwishoni mwa juma.

“Tumeanza mazoezi leo, baada ya mapumziko ya siku ya jana,nyota wetu wote wapo ikiwa ni pamoja na wale ambao hawakusafiri na timu kwenda Mwanza na Shinyanga kwenye michezo mitatu ya Mwanzo wa msimu ambayo  tuliikamilisha kwa kushinda miwili na suluhu moja,limekuwa ni jambo jema kwetu kwa sababu morari imeongezeka kikosini na kila mmoja yuko tayari kwa mchezo wa mwishomi mwa juma” alisema.

Akiendelea  zaidi Ten alisema kuwa huu ni msimu ambao City imejipanga  kuvunja  rekodi zote ambazo ilikuwa haijawahi kuzifikia tangu ilipopanda daraja  misimu mitatu iliyopita.

“Huu ni msimu ambao kwetu utakuwa na kumbukumbu nzuri kwa sababu tumejipanga kufuta ‘madeni’ yote tuliyokuwa nayo, tangu tumepanda daraja tulikuwa hatukuwahi kuongoza ligi hili sasa limeshakwisha,tunasubiri kuvunja rekodi ya kutokuzifunga Yanga na Azam fc jambo ambalo tuna amini tunalianza wikiendi hii” alitamba.

IMG_20160906_133941Geoffrey Mlawa, mazoezini leo, alipokuwa akijaribu kufanya mazoezi mepesi baadae ripoti ta daktari imesema haweza kucheza mchezo wa jumamosi dhidi ya Azam Fc kwa sababu bado ni majeruhi.

Wakati huo huo Ten ameweka wazi kuwa mshambuliaji Geoffrey Mlawa ni wazi ataukosa mchezo wa jumamosi dhidi ya Azam Fc kufuatia majeraha aliyoapata kwenye mchezo dhidi ya Toto African jijini Mwanza na tayari jopo na madaktari wa City wameshathibitisha  jambo hili mble ya benchi la ufundi.

Uwanja Wa Uhuru Kutumika Kesho
Makamu wa Rais akanusha kutaka kujiuzulu