Klabu ya Mbeya City maarufu kama Wagonga Nyundo wameanza kukiimarisha kikosi chao tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu na kombe la FA baada ya kumsajili beki wa kati wa Kagera Sugar, Erick Kyaruzi Mopa.
Kyaruzi amejiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kwa dau ambalo halijawekwa wazi.
Msimu uliopita Kyaruzi pamoja na kipa wake Hussein Sharif ‘Casillas’ walisimamishwa na uongozi wa Kagera Sugar kwa tuhuma za kuhujumu timu, walipocheza dhidi ya Young Africans na kufungwa mabao 6-2 nyumbani CCM Kaitaba.
Kyaruzi anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na Mbeya City tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa Juni 15.