Baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha, timu ya Mbeya City hatimaye imeibuka na ushindi dhidi ya JKT Ruvu katika pambano la Ligi Kuu lililopigwa kwenye uwanja wa   Karume leo jioni.

Mbeya City imefanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 ikiwa ni ushindi wake wa nne msimu huu.

Mlinzi wa pembeni, Hassan Mwasapili alitumia vizuri pasi ya Haruna Moshi kuiandikia Mbeya City bao la kwanza mnamo dakika ya 23.

JKT Ruvu walisawazisha bao mnamo dakika ya 38 kupitia kwa Yohana Morris aliyetuliza mpira kifuani kabla ya kuachia shuti kali lilomshinda kipa wa Mbeya City, Hannington Kalyesubula na kujaa nyavuni.

Furaha ya JKT Ruvu ya kusawazisha bao hilo haikudumu sana kwani dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza Mbeya City walifanikiwa kuandika bao la pili na la ushindi.

Licha ya mabadiliko kadhaa ya kipindi cha pili yaliyofanywa na pande zote,  matokeo yalibaki kama yaliyokuwa na kuipa ushindi wa nne Mbeya City.

Lukuvi awamwagia sifa Zitto na Mbatia, awaponda wengine kwa hili
Tanzania Yaendelea Kukwea Viwango Vya Ubora Wa Soka