Walinzi wa kati Tumba Sued Lui na Deo Julius (Msafa) sambamba na washambuliaji Abdalah Juma na Ditram Nchimbi ndiyo nyota  pekee ambao taratibu zao za kujiunga na City kama wachezaji wapya  kikosini tayari zimekamilika.

Mapema leo meneja usajili wa kikosi cha City, Frank Michael Mfundo amesema kuwa  licha ya nyota hao kusajiliwa bado kuna nafasi ya mchezaji mwingine kujunga na kikosi hiki kabla dirisha dogo kufungwa ifikapo desemba 15.

“Kwa mujibu wa mapendekezo ya mwalimu kwenye taarifa yake, tulikuwa na nafasi ya wachezaji watano, tayari tushakamilisha wanne ambao ni Tumba Sued kutoka Coastal Union, Deo Julius kutoka Kagera Sugar,Abdalah Juma kutoka Toto African na Ditram Nchimbi aliyekuwa Majimaji Fc  hivyo basi muda wowote kuanzia sasa nyota mwingine anaweza kuingia kikosini kukamilisha idadi ya nyota 5 waliopendekezwa na mwalimu” alisema Frank. huku akikataa kuweka wazi jina la mchezaji anayetarajia kumsajili.

Katika hatua nyingine Meneja huyo wa usajili alisema kuwa City bado haijakaa mezani  na golikipa mkongwe Juma Kaseja kuzungumza juu ya mustakabali wa mkataba wake unaofikia kikomo mwezi may mwaka huu licha ya kuwepo taarifa nyingi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Ni kweli kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu Kaseja kuongezewa mkataba, lakini kama klabu bado hatujakaa na mchezaji kuzungumza juu ya jambo hilo, hii ni kwa sababu tulikuwa na mipango mingi ya maandalizi ya duru ya pili ya msimu, hatuna shaka  kwa sababu bado ni mchezaji wetu ila muda ukifika hili litawekwa mezani na hatimaye taarifa zake kutolewa” alimaliza.

Arsene Wenger Aanza Kukiri Arsenal Yake Ina Pancha
Ruge: Hakutakuwa na Fiesta Mwaka Huu, Tumsapoti Magufuli