Kiosi cha Mbeya City kimepata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuichapa Mbao FC mabao mawili kwa moja kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mshambuliaji Peter Mapunda aliibuka lulu ya Mbeya City, kufuatia kufunga  mabao ya ushindi huku lile la kufutia machozi kwa wenyeji Mbao FC likifungwa na Emanuel Charles.

Ushindi huo unaifanya Mbeya City kufikisha alama saba sawa Young Africans huku ikijikwamua kutoka nafasi ya pili kutoka mkiani hadi nafasi ya 16, huku Mbao FC ikishuka hadi nafasi ya 17.

Katika mchezo huo Mbeya City ikiwa na machungu ya kukung’utwa mabao 4-1 nyumbani na Kagera Sugar, walihitaji ushindi ili kutetea kibarua cha Kocha wao Juma Mwambusi ambaye amekalia kuti kavu kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Mbeya City walianza kuzitikisa nyavu dakika ya 55 kupitia kwa Mapunda kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Mbao, Babilas Chitembe kumuangusha Hotikely Masasi na mwamuzi Martin Sanya (Morogoro) kuamua ipigwe penalti iliyoza bao.

Hata hivyo, Mwamuzi Sanya alimuonyesha kadi nyekundu Chitembe kutokana na rafu hiyo na kuwafanya Mbao kucheza pungufu kwa dakika hizo.

Wakati huo huo Alliance FC imeshindwa kuwia nyumbani dhidi ya Tanzania Prisons, kwa kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 29, 2019
RC akanusha kauli ya kutaka wananchi warogwe, adai kusingiziwa na upinzani