Uongozi wa klabu ya Mbeya City, umetamba kuwa na.kikosi imara ambacho kitaweza kuizuia Simba SC, katika mchezo wa kesho Jumanne (Juni 22).

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe, amesema hana shaka na kikosi chao kuelekea mchezo huo, ambao umepangwa kuanza saa moja usiku kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

Amesema baada ya kumalizana na Coastal Union ya Tanga, nguvu zao zote wanazielekeza kwa mnyama ambaye kwa kipindi hiki amekua mgumu kuangusha alama tatu.

“Tunaenda kucheza na timu bora katika ligi, lakini hilo kwetu halitutishi tuko tayari kupambana mpaka tone la mwisho,” amesema Kimbe akisisitiza benchi lao la ufundi na wachezaji wamemhakikishia Kwa Mkapa, patachimbika.

Mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine, Simba SC iliitandika Mbeya City bao moja kwa sifuri, likifungwa na.mshambuliaji na nahodha wao John Bocco.

UEFA kuchunguza vitendo vya kibaguzi
Mahakama yabatilisha uamuzi Fatma Karume kufutiwa uwakili