Baada ya safari ndefu ya saa kadhaa, kikosi cha Mbeya City FC tayari kimewasili jijini Mbeya kujiwinda na mchezo ujao  wa ligi kuu soka Tanzania  bara dhidi ya Azam FC uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine.

Muda mfupi  uliopita meneja wa kikosi hiki Geoffrey Katepa ameimbia mbeyacityfc.com kuwa Mwalimu Kinnah Phiri ameamua kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake ili waweze kupumzika kutokana na uchovu wa safari ndefu na siku ya kesho jioni wataingia  kwenye uwanja wa Sokoine  kuanza mazoezi ya matayarisho ya mchezo huo wa jumamosi.

“Mwalimu ametoa mapumziko siku ya leo hii ni kwa sababu tumekuwa na safari ndefu kutoka Mwanza tukipitia Tabora, hivyo mazoezi ya matayarisho ya mchezo ujao yataanza kesho jioni, jambo muhimu ni kwamba tunamshukuru Mungu  kwa kutuwezesha kupata matokeo mazuri kwenye michezo yetu mitatu ya mwanzo wa msimu,hili limetufanya kuongoza ligi kwa mara ya kwanza, jambo ambalo pia limetuongezea morali kubwa ya kushinda dhidi ya Azam FC jumamosi” alisema.

Akiendelea  zaidi Meneja Katepa alisema kuwa kitengo cha utabibu cha City kinachoongozwa na Dr Joshua Kaseko  kimesibitisha kuwa  wachezaji wote wako kwenye hali nzuri kwa maana ya hakuna aliye majeruhi  na baada ya mapumziko ya leo wote watakuwa tayari kwa mazoezi ya kujiandaa kucheza mchezo wa jumamosi.

“Jopo la madaktari wetu wamenithibitishia kuwa kikosini  hakuna mchezaji mwenye majeraha, wote wana hali nzuri  hivyo baada ya kupisha mapumziko ya leo wote watakuwa tayari kwa mazoezi ya matayarisho ya mchezo”. alimaliza.

Kwenye michezo mitatu iliyopita  City  ilifanikuwa kuibuka na pointi  7, kufuatia suluhu ya bila kufungana na Kagera Sugar na baadae kuiadhibu Toto Africans bao 1-0 na mwisho kuhitimisha kwa kuifunga Mbao Fc  bao 4-1 na kushika  usukuni wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Gavana wa Jimbo La Akwa Ibom Aipa Zawadi Taifa Stars
MILLIONI 30 KUGOMBANIWA NA NCHI TANO EAST AFRIKA NDANI YA MAISHA PLUS