Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa ameomba madhehebu mbalimbali ya dini yaliyopo Mikoa ya Nyanda za juu Kusini kuwasisitiza waumini wao kufanya ibada ya kusamehe hasa kwa waliopo kwenye ndoa ili kuzinusuru nyingi kati ya zilizopo kuvunjika.

Malisa ameyasema hayo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kwenye Kongamano la Kanda la kukithiri kuvunjika kwa ndoa katika Jamii, lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania – BAKWATA jijini Mbeya lililowakusanya wadau mbalimbali, ikiwemo dawati la jinsia, jeshi la Polisi na Kadhi wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini.

Amesema, ndoa nyingi za Vijana wa sasa huwa hazidumu kwa kukosa mafundisho ya mara kwa mara yatakayowafanya kuwa na uvumilivu na kusamehe.

Aidha, Malisa pia amewahakikishia waandaaaji wa Kongamano hilo kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Viongozi wa dini na kuendelea kuliombea Taifa na Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waarabu wahamishia silaha Liverpool
Maguri kuvunja rekodi Ligi Kuu 2023/24