Uongozi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA) kwa kushirikiana na wadau wa soka mkoani humo, umejipanga kuhakikisha timu za mkoa huo zinasalia Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao 2021/22.

Timu za Mbeya City na Ihefu FC zipo katika hali mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku msimu ukielekea ukingoni, hivyo zitatakiwa kushinda michezo iliyosalia ili kujinusuru kushuka daraja msimu huu 2020/21.

Uongozi wa MREFA umesema utapambana kwa kushirikiana na wadau wa Soka mkoani humo kufanikisha lengo la kuzisaidia timu hizo kubaki kwa msimu ujao, ili kuongeza idadi ya kuwa na timu tatu baada ya timu ya Mbeya Kwanza FC kupanda daraja ikitokea Ligi Daraja la Kwanza msimu huu 2020/21.

Katika Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Mbeya City FC ipo nafasi ya 13 ikiwa na alama 36, huku Ihefu ikiwa nafasi ya 15 kwa kuwa na alama 35.

Mbeya City FC inapewa nafasi kubwa ya kujitetea kutokana na ratiba kuonesha wamebakiza michezo dhidi ya Gwambina na Biashara United.

Ihefu FC ambayo inshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu msimu huu imebakiza michezo miwili dhidi ya Young Africans na KMC FC.

Manyama: Azam FC walifuata taratibu zote
KMC FC: Hatujapokea ofa yoyote