Wadau wa zao la ufuta mkoani Morogoro wamejadili mifumo ya uzalishaji na uuzaji ufuta kwa wakulima ili waweze kuzalisha kwa wingi zao hilo na kuepuka madalali kwa kuuza katika minada ili wanufaike.
Majadiliano hayo ni sehemu ya ya kuimarisha na kuboresha sera za kilimo nchini ili ziwe na tija kwa wakulima wa mazao mbalimbali.
Hayo yameelezwa na wadau mbalimbali wa kilimo katika kikao maalumu cha kupitisha mwongozo kwa wakulima wa zao la ufuta nchini.
Mwenyekiti wa kikao hicho Loatha Ole Sanare, Mkuu wa mkoa wa Morogoro amesema mazao mengi ya wakulima yanaingiliwa na madalali wanaojipangia bei kiasi ambacho ni unyonyaji mkubwa kwa walima na wanunuzi wa zao hilo.