Utafiti uliofanywa na shirika linalohusika na usalama wa wanyama duniani (World animal protection), umebaini kuwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo mbalimbali nchini wanaodhaniwa kuwa wakienyeji si kweli kama inavyosemwa.

Utafiti huo umebaini kuku hao si wa kienyeji, bali ni kuku wa kisasa maarufu kama wa kizungu wanofugwa majumbani kwa kupewa majani na dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wagumu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo uliofanyika katika nchi nne ikiwemo Tanzania, Msemaji mkuu wa shirika hilo, Victor Yamo amesema wamebaini jambo hilo hivyo walaji wawe makini.

Asema utafiti huo ulifanywa kuanzia Juni hadi Julai mwaka huu katika mikoa ya Arusha na Dar es salaam kwa upande wa Tanzania, ambapo kuku wengi wanao uzwa katika mikoa hiyo wamekuwa wakipewa dawa za kuwakuza ambazo zina madhara kwa binadamu pindi wanapotafuna mifupa.

“Wakati watu wetu wakitembelea kwenye masoko mbalimbali kuulizia bei ya kuku na aina, wakabaini uwepo wa kuku wa kisasa wengi na wananchi huuziwa kwa kuambiwa kuwa ni wa kienyeji.” amesema Yamo

Ameeleza kuwa utafiti huo ulifanyika kwa lengu la kujua walaji wananunua nyama za aina gani, kutoka wapi pamoja na kuangalia kama wanafahamu ubora wa chakula na matumizi ya dawa za wanyama.

Hata hivyo Yamo amesema kwa sasa shirika lake linafanya jitihada kubwa kuhakikisha linaimarisha ustawi wa haki za wanyama na sheria za kuwalinda wanyama hao.

 

 

Makala: Kwanini Ruiz Jr. anaweza kumpiga tena Anthony Joshua
Mvua kubwa kunyesha mikoa 9