Kampuni ya uchimbaji wa madini Tanzania – Acacia inatarajia kuzindua mashindano ya mbio za baiskeli kwa lengo la kukusanya zaidi ya Sh. milioni 340 zitakazotumika kuboresha upatikanaji wa elimu kwa jamii inayozunguka migodi hiyo iliyopo kanda ya ziwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Asa Mwaipopo Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben ambapo amesema mashindano hayo wameyapatia jina la ‘Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge’.
 
Amesema kuwa mashindano hayo yatazinduliwa rasmi Oktoba 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo na mashindano yenyewe yataanza Novemba 3 mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 
“Fedha hizo zitasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia maskini na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia sare na vifaa vingine vya shule ikiwemo vitabu na vifaa mbalimbali,”amesema Ruben.
 
Aidha, amesema kuwa hadi sasa mpango wa CanEducate ulioanza mwaka 2011, umetumia kiasi cha Sh. milioni 494 kwa kuwadhamini wanafunzi 3936, na kuziwezesha kwa njia mbalimbali shule zaidi ya tisa.
 
Naye Rais wa Chama cha Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama alitoa wito kwa wananchi na makampuni mbalimbali kujitokeza katika mbio hizo na kufadhili mpango huo ili kuiwezesha jamii kupata huduma mbalimbali za kielimu.
  • Video: Zitto, Serikali kuliamsha tena, Janga jipya lanyemelea wafiwa wa MV Nyerere
 
  • Matokeo ya darasa la saba yafutwa
 
  • Rais Magufuli na mkewe wamwaga mamilioni feri

Odinga, Ruto wamuweka njia panda Rais Kenyatta
Video: Ni ajabu na kweli bibi kizee wa miaka 72 ajifungua