Mlinda mlango wa Mwadui FC Mussa George Mbisa amefuchua siri na dhamira yake kila anapopata nafasi ya kukaa langoni.

Mbise ambaye amekua na bahati mbaya ya kufungwa mabao mengi msimu huu, amesema kila siku amekua na malengo yake binafsi, lakini hali huwa tete.

Amesema bado anaamini ana nafasi ya kutosha kuendelea kupambana ili kufikia lengo la kuwa bora, licha ya klabu yake kushuka daraja msimu huu.

“Kila ninapoingia uwanjani huwa napanga kupambana kadiri ya uwezo wangu ili kufikia melengo yangu.”

Kuhusu mchezo wa jana Jumapili (Juni 20), Mbise amesema alilua amepanga kuipambania Mwadui FC hadi dakika ya mwisho, na kwa kiasi fulani alifanikiwa.

“Nilichopanga kufanya dhidi ya Young Africans sijafanikisha kwa sababu nimeruhusu magoli matatu, lengo langu lilikuwa nisiruhusu goli lolote.”

“Kwa kiasi fulani nimejaribu, lakini nimeumizwa sana kwa kushindwa kufikia kiwango cha kuilinda Mwadui hadi mwisho wa mchezo huo.” amesema Mbise.

KUHUSU KUTAKIWA YANGA

Mbise amesema kuna baadhi ya klabu zimeonesha nia ya kumsajili.mwisjoni mwa msimu huu, lakini akasisitiza Young Africans sio miongoni mwa klabu hizo.

“Ofa zipo lakini tuzidi kusubiri, naweza kubaki Ligi Kuu au nikabaki Mwadui FC kwa sababu mimi ndio nitaamua. Kuhusu kutakiwa Young Africans hizo taarifa bado hazijanifikia.”

Chama aanza mazoezi Simba SC
Mbeya City: Tupo tayari kuivaa Simba SC