Mkongoman Dieumerci Mbokani, amekamilisha ndoto za kucheza soka nchini England, baada ya klabu ya Dynamo Kiev ya nchini Ukraine kukubali kumuachia kwa mkopo.

Norwich City klabu inayoshgiriki ligi ya nchini Engalnd ndiyo iliyofanikisha azma ya kumpeleka Mbokani nchini humo, tayari kwa mapambano ya kuwani ubingwa wa msimu wa 2015-16.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mara kadhaa alikunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari barani Ulaya, akisisiza hitaji lake la kucheza soka nchini England.

Meneja wa klabu ya Norwich City, Alex Neil amejinasibu mbele ya vyombo vya habari kwa kusema usajili wa mshambulaiji huyo utawasaidia katika harakati za kusaka mambo mazuri msimu huu na hana shaka na maamuzi waliyoyachukua.

Mbokani alianza safari ya maisha ya soka barani Ulaya akiwa nchini Ubelgiji na klabu ya Anderlecht ambayo ilimsajili kwa mkopo akitokea nyumbani kwao Jamuhuri Ya kidemokrasia ya Kongo kwenye klabu ya TP Mazembe na mwaka mmoja baadae alisajiliwa jumla na klabu ya Standard Liege kabla ya kutimkia nchini Ufaransa na kujiunga na AS Monaco.

Baadae VfL Wolfsburg ya nchini Ujerumani, walimsajili kwa mkopo kabla ya kurejea Anderlecht nchini Ubelgiji na baade alielekea nchini Ukraine kujiunga na Dynamo Kiev.

Watuhumiwa Wizi Akaunti Ya EPA Waachiwa Huru
“Msidanywe Kuhusu Sheria Ya Makosa Ya Mtandao”