Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA), Freeman Mbowe ametakiwa kumtafuta aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Wilbrod Slaa ili aweze kukiokoa chama hicho.

Hayo yamesemwa na aliyekuwa diwani wa kata ya Kimandolu, Mchungaji Rayson Ngowi, ambapo amesema kuwa kuna haja ya kutafuta hekima za Wilbroad Slaa, ili kukisaidia chama hicho kukaa kwenye mstari unaofaa, kwa kuwa sasa kimeanguka kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuwa hata yeye kutoka CHADEMA ameondoka kwa kutaka mwenyewe na sio kununuliwa kama inavyodaiwa, na kwamba kuna wengine watakaofuata nyuma yao baada ya wao kuondoka kwenye chama hicho.

“CHADEMA ya leo sio ile ya Dkt Slaa, CHADEMA ya leo ni  ya maslahi, CHADEMA ganganjaa, na wakikataa mimi nitasema, sikiliza Mbowe, chama chako kina matatizo makubwa, huna viongozi, kamtafute Dkt. Slaa nafikiri ataokoa jahazi, kama mnataka kurudisha imani, kwa sababu sio mimi tu nimeondoka watakuja wengi,”amesema Mchungaji Ngowi

Diwani amtaka Mbowe kumtafuta Dkt. Slaa
Raia wa Liberia wapiga kura kumpata rais mpya