Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu bado si nzuri kutokana na majeraha aliyoyapata.

Amesema kuwa Mbunge huyo wa Singida Mashariki bado yupo kwenye chumba cha upasuaji katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu kufuatia kiongozi huyo kupigwa risasi jana na watu wasiofahamika akiwa mjini Dodoma.

Aidha kwa upande wake mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ambaye yupo nchini Kenya amesema kuwa hali ilivyokuwa toka walipofika jana usiku nchini Kenya mpaka dakika za mwisho Mbunge huyo alipoingia kwenye chumba cha upasuaji ilikuwa bado si nzuri.

“Tundu Lisu aliwasili usiku majira ya saa saba hapa (Nairobi Jomo Kenyatta International Airport) na alipokelewa na team ya Madaktari wa Nairobi hospital pale Airport na matibabu yalianza mara moja kuanzia ndani ya Ambulance hadi hospital,” amesema Msigwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa  alipofika Nairobi hospital alifanyiwa vipimo vyote na baadae saa nne asubuhi aliingizwa chumba cha upasuaji.

Familia yamrejesha Bony Swansea City
Kukojoa kitandani ni ugonjwa wa akili