Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ameipongeza bajeti kuu ya serikali na kusema kuwa itakuwa tija kwa baadhi ya maeneo.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa ingawa kuna baadhi ya mapungufu, bajeti hiyo itaweza kusaidia baadhi ya maeneo.

Amesema kuwa bajeti iliyopitishwa ina tija kubwa ingawa iko chini ya ile ya Kenya, lakini akashauri kuwa ni vyema Tanzania ikaingiza bidhaa kutoka nchi jirani kuliko kutoka Ulaya na nchi zingine ambazo ziko mbali zaidi.

“Bajeti iko vizuri ingawa ya wenzetu Kenya iko juu yetu, lakini ningeshauri kuwepo kwa uwezekano wa kuingiza bidhaa za kutoka nchi jirani kuliko kutoka nchi za Ulaya na kwingineko,”amesema Mbowe

Hata hivyo, ameongeza kuwa bajeti ya mwaka jana haikutekelezwa kwa asilimilia mia moja ambazo walikuwa wamejiwekea.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 16, 2018
Zitto ampa tano Upendo Peneza