Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu hatasafirishwa kwenda nchi yoyote kwa ajili ya matibabu zaidi.

Mbowe amesema kuwa madaktari wa hospitali ya Nairobi nchini Kenya wanaompatia matibabu mwanasheria huyo wameeleza katika ripoti yao kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki hataweza kusafirishwa kwenda nchini Marekani au Ujerumani kama ilivyokuwa imepangwa awali, kutokana na hali yake.

Aidha, amesema kuwa Lissu yuko katika hatua ya pili ya matibabu yake na kwamba hatua ya mwisho itakamilika kwa kufanya mazoezi.

“Awamu ya tatu itaamua aende wapi, ambayo itahusisha kufanya mazoezi,” Mwananchi linamkariri Mbowe.

Lissu alishambuliwa kwa risasi zaidi ya thelathini nyumbani kwake Area D mjini Dodoma. Kati ya risasi hizo, risasi tano zilimpata tumboni, mguuni na mkononi.

Hamisa ajitapa: Baada ya Rav 4 sasa ni Prado Land Cruiser
Kiongozi wa Korea Kaskazini ajibu vitisho vya Trump, ‘itamgharimu’