Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa endapo uchaguzi utarudiwa katika kata nane ambazo madiwani wa chama chake waliojiuzuru basi taifa litaingia hasara kubwa.
Ameyasema hayo katika mikutano tofauti tofauti ya hadhara anayoifanya Jimboni kwake Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo amefafanua kuwa uchaguzi mdogo katika kata moja unatarajia kugharimu shilingi millioni 250.
Amesema kuwa kama uchaguzi ukirudiwa katika Kata zote nane ambazo madiwani wao wamejiuzuru kwa madai ya kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli, basi serikali itaingia hasara ya shilingi bilioni 2 katika kugharamia uchaguzi huo mdogo.
“Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma, kwa sababu kurudia uchaguzi mdogo katika kata moja ni shilingi milioni 250, fedha hizi zingeweza kwenda kujenga zahanati na mashule, uchaguzi ukirudiwa nitalala kila kata kuhakikisha haiendi popote,”amesema Mbowe
Aidha, kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa hawezi kuongelea suala hilo kwakuwa yeye sio mwanasiasa hivyo hawezi kuzungumzia chochote.
-
Mbowe amkumbuka Kikwete, asema hali kwa sasa ni tete
-
Mbowe: Kilimanjaro hatutegemei CCM kuleta maendeleo
Hata hivyo, kata nane za madiwani wake walijiuzuru na kumuunga mkono Rais Maguli ni pamoja na kata tatu za jimbo la Hai, kata nne za jimbo la Arumeru Mashariki na moja iliyopo Arusha Mjini.