Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa hali yake kiafya inaendelea vizuri baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa amelazwa tangu juzi.

Akiongea na waandishi wa habari katika hospitali hiyo ya Taifa, Mbowe alieleza kuwa uchovu ndio sababu kubwa iliyopelekea kuugua ghafla katika maandamano ya kumsindikiza Lowassa baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais katika ofisi za Tume Ya Taifa.

“Nililazimika kuja hospitali kwa sababu ya kupata medical attention, baada ya kuwa na kabilio la kizunguzungu kikubwa. Na vipimo vya madaktari vilinitaka kwanza nipumzike kwa masaa 48, na majibu ya kiuchunguzi wa madaktari yalibainisha kwamba nilikuwa nasumbuliwa na matatizo mawili; la kwanza ni exhaustion na la pili ni fatiki. Kwamba kwa muda mrefu nimekuwa nafanya kazi usiku na mchana,” alisema Mbowe.

Naye mganga aliyemhudumia mwanasiasa huyo, Shemu Tulizo alithibitisha kuwa matatizo aliyoyaeleza Mbowe mbele ya waandishi wa habari ndiyo yaliyobainika baada ya uchunguzi na kwamba alipofikishwa hospitalini hapo alipewa huduma chini ya jopo la madaktari watano.

Daktari Tulizo alisema kuwa mwanasiasa huyo anaendelea vizuri na angeruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya masaa 48 kuanzia juzi.

mbowee

Mbowe aliishiwa nguvu wakati akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, kuchukua fomu juzi, akiwa katika eneo la Manyanya, Kinondoni na kulazimika kukimbizwa Muhimbili.

Daktari Eva Carneiro Apigwa Stop Chelsea
Team Messi Waitambia Team Ronaldo Mitandaoni