Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa amesikitishwa sana na namna kesi yao inavyoendeshwa, huku akiongeza kuwa hawaogopi kwenda jela bali wanataka wafungwe kwa haki.

Amesema kuwa hawaamini katika mapambano ya ngumi, bali wanaiamini sheria na kuiomba mahakama itende haki dhidi ya mashtaka yanayowakabili.

“Hatuoni haki ikitendeka katika kesi inayoendeshwa na Hakimu Mashauri, kesi inaendeshwa kwa maelekezo ili sisi tuonekane tuna hatia, sisi hatuhusiki na mauaji ya Akwilina, wanaohusika wao wenyewe wanawafahamu na walikuwa wanachunguza , nachotaka kusema sisi hatuogopi jela, lakini tunataka tufungwe kwa haki,”amesema Mbowe

Aidha, kauli hiyo imejiri mara baada ya Wakili, Jeremiah Mtobesya aliyekuwa akiwawakilisha Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na viongozi wenzake nane wa chama hicho kujitoa.

Mtobesya amejitoa katika kesi hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Kisutu kutupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 iahirishwe katika Mahakama ya Kisutu.

 

 

Waziri Mkuu wa Australia ang'olewa madarakani
Afrika Kusini yamtaka Rais Trump kuacha uchochezi