Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo atazungumzia kinachoendea katika hospitali ya Narobi nchini Kenya kuhusu afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chama hicho, Tumaini Makene, Mbowe atazungumzia hayo leo katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Mbowe anatarajia kuzungumzia michango iliyokusanywa na matumizi yake.

“Kupitia kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, chama kitatoa taarifa kuhusu maendeleo ya Tundu Lissu, mrejesho wa michango na gharama za matibabu,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa mkutano huo utafanyika majira ya saa tano asubuhi.

Lissu anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kushambuliwa na risasi akiwa ndani ya gari, nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma.

Jana, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliwaambia watanzania kupitia Instagram kuwa alimtembelea Lissu na kuliona tabasamu lake, hivyo akawasihi waendelee kumuombea.

Major Lazer waachia video ya ‘Particula’ wakiwa na Dj Maphorisa, Nasty C, Ice Prince, Patoranking na Jidenna
Fid Q afunguka kuhusu mpango wa kuingia kwenye siasa