Viongozi wa upinzani akiwemo Freeman Mbowe na Profesa Ibrahim Lipumba leo katika sherehe za Uhuru Jijini Mwanza, wamekutana na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, na amewapa nafasi ya kutoa salamu ambopo wote wameomba amani na demokrasia kudumishwa.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania, Mbunge wa Hai Freeman Mbowe wakati akitoa salamu zake kwa wananchi, amemuomba Rais Magufuli, kutumia siku hiyo kuleta maridhiano yenye mshikamano na upendo, yatakayoleta amani na Demokrasia kwa Taifa.

“Ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango, tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu Demokrasia, tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano na Mh. Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa, kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia, kaliweke Taifa katika nafasi ya utengamano” amesema Mbowe

Kwa upande wake Profesa Lipumba amesema kuwa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, lipo jukumu la kuhakikisha Demokrasia inakuwepo.

“Natoa pongezi kwa Watanzania wote, kwa kusherehekea miaka 58 ya Uhuru, mimi nilikua naingia darasa la nne, nampongeza Rais kwa kazi aliyoifanya, namuomba ajue anajukumu la kujenga demokrasia kwenye nchi yetu kuelekea Uchaguzi 2020” Amesema Profesa Lopumba

New Zealand: Volkano yalipuka kisiwa cha watalii
Kwa mara ya kwanza mlimbwende mweusi kutoka Afrika kusini atwaa taji la 'Miss Universe' Dunia