Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Machi 10, 2020 imewahukumu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake kulipa faini ya sh. Mil 350 au kwenda jela miezi mitano, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 ikiwemo la kufanya maandamano bila kibali.

Hukumu hiyo iliyochukua takribani saa 4, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 11 jioni, ilisomwa na Hakimu Makazi wa Mahakama hiyo Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema washtakiwa hatiani katika mashitaka 12 kati ya 13, kosa ambalo hawajatiwa nalo hatiani ni kosa la kwanza ambalo ni kufanya mkusanyiko usio halali.

Aidha, Hakimu Simba ameeleza kuwa katika shtaka la pili la uchochezi lililokuwa likiwakabili watuhumiwa wote, kila mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 10 au kwenda jela miezi mitano. Katika shtaka la 3 hadi 6, mahakama imeamuru kila mshtakiwa kulipa faini ya Shilingi milioni 10 au jela miezi mitano.

Hata hivyo, shtaka la 9, 10 linamhusu Mbowe peke yake, hivyo kila kosa atalipa Tsh milioni 5 au jela miezi mitano na katika shtaka la 11 atalipa faini ya Sh 10 milioni.

Katika adhabu ambayo, Mbowe amehukumiwa ni kulipa Sh.Mil 70, Halima Mdee Sh.Mil 40, Dkt. Mashinji kulipa Sh.Mil 30, John Heche Sh.Mil 40, Msigwa Sh.Mil 40, Bulaya Sh.Mil 40, Mnyika Sh.Mil 30, Salum Mwalimu Sh.Mil 30 na Ester Matiko Sh.Mil30.

 

 

Video: Undani wa hukumu ya kina Mbowe, Membe ahoji mchakato kufukuzwa kwake CCM
Rais Xi Jinping atembelea Wuhan mji ulioathirika zaidi na Corona