Wabunge 15 wamezuiliwa kuingia bungeni kuanzia kesho Mei 15, 2020 mpaka hapo watakapotimiza masharti ya kurejesha fedha za posho na wawe na majibu ya vipimo vya ugonjwa wa Corona.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Spika wa Bunge, Job Ndugai ameagiza kitengo cha usalama cha bunge kutowaruhusu wabunge hao kuingia bungeni.
Wabunge hao ni pamoja na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Ester Bulaya (Bunda), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Joseph Mbilinyi (Mbeya), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Rohda kunchela na Pascal Haonga.
Wengine ni Catherine Ruge, Devotha Minja, Joyce Mukya, Aida Khenan, Upendo Peneza, Grace Kiwelu na Joseph Haule.
“Ofisi ya bunge inatoa taarifa kwamba katika siku za hivi karibuni baadhi ya wabunge wa Chadema wamekuwa watoro kwa kutohudhuria vikao vyake bunge bila ruhusa ya Spika kwa muda wa wiki mbili kinyume na masharti ya kanuni ya 146 inayosisitiza wajibu wa kila mbunge kuhudhuria vikao vyake bunge,” taarifa hiyo imeeleza.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa wabunge hao walisusia vikao vya bunge huku wakiwa wamelipwa posho ya kujikimu ya kuanzia Mei 1 hadi 17, 2020 hata hivyo Spika Ndugai amewataka wabunge hao kurejea bungeni au kurehesha fedha walizolipwa mara moja.
Ayoub Lyanga: Young Africans hawatimizi ahadi, nitakwenda Serbia
Visa vya corona vyafika 737, visa vipya 22 vyabainika – Kenya