Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi imewakuta washtakiwa wote wanne akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake wana Kesi ya kujibu kwa mashtaka matano ambapo la sita Mahakama imelitupilia mbali baada ya mahakama kujiridhisha hivyo chini ya Jaji Joachim Tiganga.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga ambapo amesema Mahakama imepitia ushahidi wote wa Jamhuri wa Mashahidi 13 ambao umewafanya Washitakiwa wakutwe na kesi ya kujibu.

Hata hivyo Mahakama hiyo imemuachia huru Mshtakiwa wa kwanza baada ya kutokuwa na kesi ya kujibu katika shitaka la sita la kukutwa na sare na vifaa vya Jeshi licha ya kwamba atajitetea katika makosa mengine.

“Katika shitaka la 6 linalomkabili Mshtakiwa wa kwanza hajakutwa na kesi ya kujibu, hivyo katika kosa hilo yupo huru”

Zimetimia siku 202 tangu kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu ianze katika Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Agosti 31, 2021

Habari picha: Rais Samia afanya mazungumzo na Rais wa Kamisheni EU
Rais Mwinyi afanya uteuzi mwingine