Mahakama kuu leo kitengo cha ardhi kitatoa uamuzi wa kupigwa au kutopigwa mnada mali, baada ya mwenyekiti huyo kufungua kesi ya kupinga Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kumwondoa kwenye jengo lake.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na jaji Siyovelwa Mwangasi, baada ya kupitia hoja zilizotelewa na mawakili wa Mbowe na mawakili wa NHC.

Shirika hilo lilichukua mali za kampuni za Mbowe kupitia mawakala wa Fosters Auctioners katika jengo lilipo makutano ya mataa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya).

Hatua hiyo ilitokana na mgogoro wa muda mrefu, ikimtuhumu Mbowe , kushindwa kulipa deni la zaidi ya sh bilioni 1.3 ikiwa ni jumla ya fedha za kodi ya kupangishwa kwenye jengo hilo.

Dirk Kuyt: Kauli Ya Pogba Ilinishangaza
Madereva wa Malori wa Tanzania, Kenya waliotekwa Kongo waokolewa