Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua hukumu ya kesi ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na wenzake, na kuamuru warejeshewe kiasi cha shilingi milioni 350 walicholipa kama faini.
Uamuzi huo umetolewa leo Juni 25, na Jaji wa mahakama hiyo Irvin Mgeta, aliyesikiliza rufaa hiyo amekubaliana na rufaa hiyo baada ya kuridhika na hoja za rufaa zilizowasilishwa na wakili wa Peter Kibatala na ikatengua hukumu ya Mahakama ya Kisutu.
Katika hukumu hiyo Jaji Mugeta amesema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthitisha baadhi ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili warufani hao kwa kiwango kinachotakwa kisheria yaani bila kuacha mashaka yoyote na kwamba mashtaka mengine yalikuwa na kasoro za kisheria.
Mbowe na wenzake walitiwa hatiani na kuhukumiwa kulipa faini hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopo mkoani Dar es salaam.