Mbunge kutoka Nchini Rwanda Gamariel Mbonimana amejiuzulu, baada ya kuendesha gari akiwa amelewa ambapo ameomba umma msamaha pamaoja na Rais wa Nchi hiyo Poul Kagame, na kusema kuwa ameamua kutokunywa tena pombe.
Mbunge huyo ambaye alijiuzuru Novemba 14, 2022, hakueleza zaidi kuhusu hatua yake huku Bunge la Rwanda likiidhinisha kujiuzulu kwake na kutaja sababu za binafsi za kujiuzulu.
Hii inajiri siku moja baada ya Rais Paul Kagame kumkosoa mbunge ambaye hakumtaja jina, kwa kuendesha gari akiwa mlevi. Rais Kagame pia aliwashangaa Polisi kwa kutomkamata mbunge huyo kwa sababu ya kuwa na kinga.
Kagame alisema kuwa na kinga sio sababu ya mtu kutenda kosa na pia alilaumu mamlaka ya usalama kwa kutompokonya leseni yakena kuongeza kuwa gari ukiwa mlevi inahatarisha maisha ya dereva na umma.
Kupitia ukurusa wake wa Twitter Mbonimana ameandika kuwa “Kutoka ndani ya moyo wangu, naomba radhi kwa Rais wa Jamhuri na umma kwa ujumla. Ilikuwa makosa kwangu kuendesha gari nikiwa mlevi. Nimeamua kuacha unywaji pombe kuhusiana na suala hili. Kubali ombi langu. Nikikabidhiwa kazi nyingine, nimejitolea kutimiza majukumu mengine yoyote,” alisema Mbonimana akikiri kujutia kuvunja sheria za barabarani kwa kuendesha gari akiwa mlevi.
Inaripotiwa kwamba Mbonimana amekamatwa mara sita katika nyakati tofauti na polisi akiendesha gari akiwa mlevi kosa ambalo ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo ripoti zinaonyesha kuwa, mara zote, alitoroka polisi kwa kutumia wadhifa wake wa kuwa mbunge mwenye kinga.
Mbonimana amehudumu kama mbunge tangu mwaka wa 2018, na ni mwanachama wa Liberal Party, ambacho ni chama mshirika wa chama tawala cha Kagame, RPF.