Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene kuwaruhusu Wakulima wa bangi kuiuza katika kipindi cha miezi sita.

Amesema, wapo Wakulima wa bangi wanaoshindwa kuiuza kwa kuwa kilimo hicho hakiruhusiwi nchini, na kumuomba waliolima wapewe msamaha wa miezi sita ili wauze kabla soko la zao hilo kuporomoka

Mbunge huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akiitaka Serikali kuruhusu kilimo hicho akidai kina soko kubwa ndani na nje ya Tanzania, ametoa kauli hiyo leo.

Baada ya kauli hiyo, Spika Job Ndugai ameisihi Serikali kuangalia jambo hilo kwa mapana kwani nchi ya Canada inapata fedha nyingi kupitia zao hilo

Rais wa zamani wa Kenya, Daniel Moi afariki dunia, fahamu mwenendo wa afya yake
RC alizwa na maiti za vichanga wakati wa kuaga miili ya waumini 20 Moshi