Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM) Husna Mwilima amesema kuwa wahudumu wa ndege walioajiriwa na shirika la Ndege nchini (ATCL) hawana mvuto kwa wateja.

Ameyasema hayo leo Novemba 7, 2019, Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya mpango wa Taifa wa maendeleo, licha ya kutoa pongezi kwa Rais John Magufuli kwa kukamilisha ahadi yake ya kufufua shirika hilo.

Mwilima alijihami kwanza kwa kusema kuwa anataka kutania kidogo juu ya wahudumu wa ndege za ATCL.

“Mheshimiwa Waziri, mimi nataka nitanie kidogo hizi ndege zetu zinafanya vizuri sana lakini mle ndani hebu tuangalie tunao waajiri” amesema na kuongeza kuwa.

“Sijui mnatumia vigezo gani? unakuta Air hostless mfupi, hana mvuto wakuifanya ndege zetu zionekane. Leo mimi hapa nimezeeka ninamiaka 50 na ukiniweka…” kabla ya kuendelea kuzungumza alikatishwa na utaratibu ulioombwa na Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma.

Msukuma amedai kuwa kauli aliyotoa Mbunge huyo ni ubaguzi kwani kuna wengine wanazaa watoto ambao hawana maumbo kama anayoyataka Mbunge Mwilima yawe vigezo vya kuajiri wahudumu wa ndege za ATCL.

Aidha Mbunge Mwilima aliendelea na kutoa msisitizo kuwa mhudumu wa ndege ni lazima awe mrefu na amenyooka, akiwa mwanamke au mwanaume, na ameomba jambo hilo lizingatiwe.

Kamati ya mashindano Young Africans yavunjwa
Mwenyekiti auawa akitatua mgogoro wa Aridhi Kiteto