Rekodi mpya barani Afrika imewekwa na Mbunge wa nchini Zimbabwe, Joseph Chinotimba aliyembusu hadharani mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kutokea barani Afrika.

Chinotimba ameingia kwenye rekodi baada ya kufanya tendo hilo na mkewe katika hafla iliyofanyika jijini Harare siku ya Valentine (Februari 14) iliyoandaliwa na ‘Daftari la Rekodi Barani Afrika’.

Mbunge Zimbabwe 2

Chinotimba alimpiga busu mkewe kwa dakika 10 na sekunde 17 bila kuacha nafasi huku umati uliohudhuria ukiwashangilia, na mwisho kukabidhiwa rasmi tuzo hiyo.

Hafla hiyo ilikuwa sehemu ya kusherehekea siku ya Valentine.

Tailor Swift ampiga ‘vijembe’ Kanye West baada ya Kushinda Tuzo ya Grammy
Picha, Orodha Kamili ya Washindi wa Tuzo za Grammy 2016