Mbunge wa Nanyamba kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi, Abdallah Chikota amemtaka waziri wa fedha na mipango Philip Mpango kutoingia katika historia ya kuliua zao la korosho.

Kutokana na hoja ya serikali ya kurudishwa asilimia 65 ya ushuru unaotokana na mauzo ya korosho nje ya nchi, mbunge huyo alisema uwekezaji uliofanyika katika kwa miaka mitatu iliyopita uliinua zao hilo lakini kwa sasa anasikitishwa na mambo yanayolenga kudhoofisha zao hilo.

Mbunge huyo aliongeza kuwa yeye na wabunge wa Kusini walikwenda kwa waziri wa fedha na mipango kuzungumzia upatikanaji wa fedha za pembejeo na aliwajibu kuwa kuna tatizo katika sheria ya korosho kwa sababu ilipaswa kuanza kutumika baada ya kutengenezwa kanuni..

”Sheria ya korosho ambayo inasema asilimia 35 ya ushuru wa mauzo ya nje ( Export Levy) itakwenda mfuko mkuu wa serikali inakwenda kufutwa na nimechungulia katika muswada wa sheria ya fedha (Finance Bill) inafutwa ili pesa zote ziingie katika mfuko mkuu”, alisema Chikote.

Aidha mbunge huyo alisema kuwa madhara ya kukosekana kwa fedha hizo ni upungufu wa miche ya korosho na kushindwa kuendeleza maeneo mapya na kupotea kwa ajira za watumishi.

 

 

 

Mke wa Waziri Mkuu Israel ashtakiwa kwa ufisadi
Barcelona, Gremio kukamilisha dili la Arthur de Oliveira Melo