Mbunge wa Kilombero kupitia tiketi ya Chama cha Demikrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Lijualikali amemwaga machozi bungeni akidai kuadhibiwa na chama chake, ambapo amemuomba Spika Ndugai kujiunga na CCM kwa kusema yupo tayari kupewa kazi yoyote.
Amesema kuwa kila mwezi Wabunge wa CHADEMA wanakatwa Tsh. Laki tano, kuchangia mfuko wa chama wakati wa kampeni, fedha zilipofika Tsh. Bilioni 8 na walipohoji hizo fedha zipo wapi wakajibiwa uchaguzi ni mchakato.
Ameongeza kulalamika kuwa “Nimefungwa miezi sita jela kwa sababu ya kukitetea chama changu, halafu leo eti wanasema nimerudi Bungeni kwa sababu ya posho”.
“CHADEMA tumekuwa tukipigania uwepo wa Katiba ya nchi wakati Katiba yetu ya chama hatuifuati.” amesema Lijualikali
Aidha amefunguka kuhusu karantini” Nilipohoji ndani ya chama changu kwamba baada ya kukaa karantini, tukirudi Bungeni tunarudi kwa hoja gani? Sikupewa majibu. Wabunge wa CHADEMA tunashindwa kumweleza Mwenyekiti kama anakosea. Hatuwezi kuwa wanademokrasia kama sisi hatuna Demokrasia”