Aliyekuwa mbunge wa Mtambile kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Abdallah Salim amefariki dunia leo Julai 25, 2022 katika hospitali ya rufaa ya mkoa Pemba, visiwani Zanzibar.

Katibu wa Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Salim Bimani amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanasiasa huyo ambaye amefariki leo asubuhi kutokana na maradhi ya moyo.

Bimani amesema mazishi ya Masoud yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwake Mtambile, saa 10 jioni ya leo baada ya sala ya alasiri.

Hadi anafikwa na umauti, Masoud alikuwa msemaji wa kisekta wa ACT Wazalendo katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Itakumbukwa, Salim amekuwa mbunge wa Mtambile kupitia CUF kuanzia mwaka 2003 – 2020 na katika Bunge lililopita alikuwa mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kabla ya kuhamia ACT Wazalendo mwaka 2020 kumfuata Maalim Seif Sharif Hamad.

Madereva watakiwa kujiepusha na migomo
Geita Gold yapewa mchongo CAF