Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Wananchi ameshiriki katika hatua za awali za ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Msembeta, Kata ya Chigongwe Jijini Dodoma.

Mavunde alikutana na kuzungumza na Wananchi April 06/2019 alipofanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa mtaa huo akisikiliza kero zao ndipo alikutana na hoja ya ukosefu wa Zahanati jambo lililomlazimu Mbunge huyo kuahidi kuanzisha ujenzi wa Zahanati hiyo.

Aidha, pamoja na kushiriki zoezi la kuchimba msingi wa zahanati hiyo akishirikiana na wananchi pia amekabidhi mifuko ya Saruji 100 na kuahidi kusimamia ujenzi huo hadi Zahanati hiyo itakapo kamilika ili kuondoa adha ya wakazi zaidi ya 2300 ambao wanatembea umbali wa kilomita 10 kufuata huduma za Afya katika maeneo jirani.

Akishukuru kwa niaba ya wananchi, Esther Masimami amempongeza Mbunge Mavunde kwa kuanzisha mchakato huo wa ujenzi wa Zahanati ambao utawapunguzia adha kubwa ya ukosefu wa huduma ya Afya kwa wakati na kuahidi kujitolea katika nguvukazi kama sehemu ya mchango wao kwenye zoezi hilo.

“Sisi Wananchi tunampongeza sana Mbunge wetu Mavunde kwa kukiona kilio chetu na kuanza kukitatua leo amefika hapa na kushirikiana na sisi kuchimba msingi wa Zahanati, pia ametukabidhi Saruji mifuko 100 ya kuanzia kazi, sisi tunaahidi kutoa nguvu zetu ili kukamilisha kazi hii” amesema Mwananchi Huyo.

Madiwani wamvaa Mkurugenzi Makambako, ' Huyu hatufai'
Agizo la Rais Magufuli Njombe latekelezwa