Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo, kwa tuhuma za kuhusika kwa tukio la kufungwa kwa njia kwenye barabara ya kuelekea kwenye mgodi wa GGM.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamanda Mponjoli Mwabulambo ambapo amesema kuwa Musukuma amekamatwa leo baada ya kupata taarifa kuwa anahusika na tukio hilo.

“Ni kweli Mbunge Musukuma tumemkamata leo kufuatia tukio la juzi ambalo amehusika katika kuhamasisha kufungwa kwa barabara hiyo, hivyo tuko naye kwaajiri ya mahojiano,” amesema Kamanda Mwabulambo

Aidha,  Mwabulambo amesema mpaka sasa wanawashikilia watu 8 ambao 6 miongoni mwao ni madiwani wa kata mbali mbali mkoani humo, na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kama ambavyo inatakiwa.

Hata hivyo, Siku ya Alhamisi ya Septemba 14, 2017, wananchi mkoani Geita walifunga barabara inayoingia katika mgodi wa GGM kushinikiza malipo ya kodi.

Hamiliton azidi kung'ara mbio za Singapore Grand Prix
Video: Makonda kuwakwamua watumishi wa umma jijini Dar