Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe, Neema Mgaya ametoa Vifaa vya michezo kwa timu tatu za mpira wa Miguu zilizopo mkoani humo.

Mbunge huyo amekabidhi Jezi kwaajili ya Timu za mpira wa Miguu katika Kata ya Lubonde, Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Mapinduzi Queens iliyopo Wilayani Ludewa, Mwembetogwa FC na Majengo FC zilizopo Mjini Makambako na Yakobi, ambapo vifaa hivyo, vimegharimu kiasi cha Shilingi milioni moja Tsh. 1,000,000/=

Akiwa katika Kikao cha Baraza la Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM (UWT) wilaya ya Ludewa Mbunge huyo amemkabidhi Jezi Katibu wa CCM wilayani humo, Bakari Mfaume kwaajili ya Timu ya Wanawake ya Mapinduzi Queens ambayo ipo chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Njombe.

Aidha, Timu za Mwembetogwa FC na Majengo FC zilizopo Mjini Makambako wakati wa kupokea Vifaa hivyo, ziliwakilishwa na baadhi ya wachezaji wake wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe, Rosemary Lwiva ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana wa timu hizo mbili.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha kutoa vifaa hivyo, Mgaya amesema kuwa lengo ni kuhakikisha Sekta ya Michezo mkoani Njombe inakua, pamoja na kukuza vipaji vya vijana ambao wameamua kujiingiza katika Michezo.

Mnatakiwa kujivunia miradi inayotekelezwa na serikali- Omary Mgumba
Video: Tazama viwanda 500 vya kuchakata mabaki ya miti Tanzania vitakavyofanya kazi, Ajira kedekede