Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya CCM, Mrisho Gambo amekagua maduka ya wafanyabiashara katika soko la Kilombero na kituo cha mabasi madogo yaliyofungwa baada ya wapangaji kushindwa kulipa kodi kwa wakati.

Aidha, Serikali ilitoa maelekezo kuwa biashara za wanaodaiwa kodi zisifungwe na badala yake mamlaka husika zikae na wafanyabiashara na kujadiliana.

Akizungumza na wafanyabiashara hao, Gambo amesema walikubaliana na viongozi wa Jiji pamoja na Mkuu wa wilaya maduka hayo yafunguliwe ili kuwapa nafasi wafanyabiashara walipe madeni yao.

Akiwa katika soko hilo leo Desemba 23,2020 alielezwa na mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo, Abdi Mchomvu kuwa maduka 15 yamefungwa licha ya mkutano walioufanya na mkurugenzi wa Jiji Desemba 16,2020 kumwomba waendelee kufanya biashara huku wakilipa malimbikizo ya kodi za nyuma.

“Jambo la kusikitisha tangu tumemaliza kikao kile zimepita zaidi ya siku tano sasa maduka bado hayajafunguliwa na kipindi hiki ni cha sikukuu ambacho wafanyabiashara wengi wananufaika kibiashara,” amesema Gambo.

Trump agoma kuidhinisha Dola Bil. 900 kuwasaidia waathirika wa Corona
Melfu waandamana wakitaka Waziri mkuu ajiuzulu