Mbunge wa Jimbo la Mchinga lililopo mkoani Lindi kupitia tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Hamidu Bobali amemuomba Rais Dkt. John Magufuli, kuingilia kati na kuona jinsi agizo la Rais mstaafu Jakaya Kikwete alilolitoa mwaka 2010 lilivyopuuzwa kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Lindi.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka 2017/18, liliamua hospitali hiyo kujengwa Kata ya Kiwalala bila kujali kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ulikuwa ni utekekezaji wa agizo la Rais.
“Kwa mujibu wa kanuni, Rais akitoa maagizo ya jambo fulani litekelezwe, hakuna mtu au kundi la watu ambao wanaweza kutengua maamuzi hayo isipokuwa Rais mwenyewe. hivyo basi huwezi kubadilisha jambo hilo kama Rais hajatengua, sasa tunashangaa huu ujasiri wa kubadilisha ujenzi wa kituo cha afya wanaupata wapi,” amesema Bobali
-
Bei ya mifugo yapaa sokoni
-
NBS kujenga kituo kimoja cha Takwimu za Afya
-
Ndugulile apiga marufuku watu kujipima Ukimwi
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kitomanga, Hamisi Msagula (CUF), amesema kuwa kituo hicho cha afya ambacho kilitarajiwa kuwa hospitali ya wilaya, kingekuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo yake, vijiji na vitongoji mbalimbali vya Halmashauri ya Lindi.