Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ameomba umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA katika jimbo la Geita Mjini kwa vile katika jimbo hilo kuna kata mbili tu ikiwemo Kalangalala na Bombambili na maeneo yote yaliyobaki ni vijiji.
Amemuomba Waziri wa Nishati, Dkt.Medald Kalemani kuharakisha zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo ya yaliyoyopitiwa na umeme huo kwa vile tokea mradi huo ulipozinduliwa mwaka jana, kijiji kimoja tu katika jimbo hilo ndio kimenufaika na mradi huo.
Akizungumza kabla ya kuzindua umeme wa REA katika kijiji cha Ibanda wilayani Geita, Dkt. Kalemani ametaja sababu zilizoifanya Geita Mjini kuchelewa kupata umeme wa REA kwa vile Geita mjini inahesabika kuwa ni mjini na mjini hakuna vijiji bali kuna mitaa.
“Sisi tuliambiwa tupeleke umeme kwenye vijiji na sio kwenye mitaa, Kanyasu ndio kapigania kutuambia kuwa hii sio mitaa ni vijiji,”amesema Dkt. Kalemani
Aidha, Dkt. Kalemani amemhakikishia Mbunge huyo kuwa jumla ya vijiji 42 tayari vipo kwenye mpango wa kuunganishwa na mradi wa umeme wa REA.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kalemani amepiga marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme kiasi cha fedha kinachozidi shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atakayetozwa zaidi ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukuliwa.
-
Video: Prof Lipumba apata pigo la kwanza CUF, DCI afunguka shambulio la Tundu Lissu
-
Mwanjelwa ang’aka, ‘Nataka uache kiburi’
-
Kangi Lugola amng’oa mkuu wa kituo cha Polisi Mang’ola
Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa umeme kwa gharama hizo kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirika la umeme Tanzania(TANESCO