Mbunge wa Jimbo la Kibaha mkoani Pwani, Sylivester Koka ametoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 400 ambavyo vitasaidia kupunguza kero ya kukosa tiba kwa wananchi wa jimbo hilo.
Koka amesema kuwa vifaa hivyo vipo 831 na vitagawiwa katika kituo cha afya cha Mkoani na Zahanati 11 zilizopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Ameongeza kuwa amefanikiwa kupata vifaa hivyo kupatia shirika na la Project Cure na marafiki zake walioko nchini Marekani ambao wanafadhili vifaa tiba kwa nchi zinazoendelea.
“Nimeamua kuwatumikia wananchi wangu kwa kufanikisha vifaa hivyo na hatimaye vimepatikana na kama mnavyoona viko ,” amesema Koka.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa vifaa hivyo ni vya kisasa na watumishi wa Idara ya afya wanapaswa kuvitumia vizuri ili viwe na manufaa na kuondoa changamoto zilizopo.