Mbunge wa Jimbo la Kindondoni kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia amejiuzulu Ubunge na uanachama wa chama hicho na nafasi zote za uongozi alizokuwa nazo.

Amesema kuwa sababu kubwa ya yeye kuamua kujiuzulu nafasi hiyo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Magufuli baada ya kuona kwamba anafanya na kutekeleza mambo mengi ambayo upinzani uliahidi kufanya.

“Nimeamua kujiuzulu nafasi zote ili kuweza kuungana na Rais Dkt. Magufuli kwakuwa anatekeleza mambo mengi ambayo upinzani uliahidi kuyafanya,”amesema Mtulia

Aidha, amesema kuwa ataendelea kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Kinondoni kama kawaida katika kuwaletea maendeleo.

Video: Mbunge Nassari alivyonusurika risasi 13, Diallo akerwa Takukuru kumpekua
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 3, 2017